WAFANYABIASHARA WA MADINI WALALAMIKIA KUDAIWA TOZO MARA MBILI KWA MWAKA


Chama cha wanunuzi na wauzaji wa Madini Tanzania TAMIDA kimetoa tamko la kulaani kitendo cha uongozi wa Haliamshauri ya Simanjiro kuwavamia wafanyabiashara wa madini wa jijini Arusha maofisini wakiwa wameambatana na Askari wenye silaha za <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
moto na pingu kuwalazimisha kulipa kodi ya tozo ya huduma ya Madini.


Akitoa tamko hilo katika mkutano wa wafanya biashara wa Madini uliofanyika katika Ofisi za wizara ya madini Kanda ya Kaskazini jijini hapa Makamu mwenyekiti wa TAMIDA Thomas Munis alisema kitendo hicho hakikubaliki na kimelenga kuwadhalilisha wafanyabiashara hao pamoja na wateja wao.
Thomas aliutaka uongozi wa Wilaya ya Simanjiro kukaa chini na kukubaliana namna ya ulipaji wa tozo hiyo inayofikia kiasi cha shilingi Milioni 20 hadi 60 kwa mwaka, jambo ambalo alisema hawawezi kulipa mara mbili kwa halimashauri ya Arusha pamoja na Halimashauri ya Simanjioro.
"Sisi kama wafanyabiashara hatupingi kulipa kodi yoyote ya madini ila tunachosikitishwa nacho ni hatua ya uongozi wa Simanjiro kutufuata maofisini wakiwa na silaha za moto na pingu, kutaka tulipe kodi huduma ambayo kimsingi tumekuwa tukilipa kila mwaka katika halimashauri ya Arusha", Alisema Thomas.
Aidha aliongozea kusema kuwa wao kama wafanyabiashara wa madini hawapingi kulipa kodi yoyote inayotozwa kutokana na biashara ya madini ila wanachopinga kodi hiyo kutozwa mara mbili kwa mwaka katika halimashauri zote swala ambalo wameliomba serekli kupitia wizara ya madini kuingilia kati swala hilo na kutatua mkanganyiko huo.


Wakati huo huo afisa madini kutoka ofisi hiyo ya kanda Bwana Erick Mpesa amesema kuwa wao kama kama wasimamizi wa madini katika kanda hii wanangoja maafikiano ya pande zote mbili ikiwemo halmashauri ya Simanjiro pamoja na jiji la Arusha juu ya Tozo hiyo ya huduma ya Madini.
Kwa upande mwanasheria Jiji la Arusha Bahati Chojo amesema kuwa sheria inaelekeza wazi kuwa kampuni yoyote inayofanya biashara ya madini inapaswa kulipa tozo ya huduma kule ilipo ikiwemo kulipa kule ilipo ofisi pamoja na maeneo ya matawi ya ofisi hizo.







Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top