Video: MCHEZAJI WA BOSNIA AWATEMBEZEA MAKOFI FABREGAS NA AZPILICUETA

Mchezo kati ya Uhispania na Bosnia uliopigwa jana ulikuwa ni wa kirafiki kama ilivyo kawaida kwa timu nyingi kwa sasa lakini, lakini ulikuwa tofauti kidogo kwa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
mchezaji wa Bosnia Emir Spahic.

Mchezaji huyo wa zamani wa Sevilla alionekana kuwa na bifu na baadhi ya wachezaji wa Uhipania, na kufanya mambo yasiyotarajiwa kwa wachezaji wenzake ikilinganishwa na lengo la mchezo huo ambao ulikuwa ni wakirafiki.

Wakati Hispania wakiwa wanaongoza magoli 2-1 wakati wa kipindi cha kwanza, Spahic alijikuta akifanya mambo ya ajabu baada ya kuwazaba makofi Azpilicueta na Cesc Fabregas, ambapo kwa upande wa Fabregas alifanyiwa hivyo baada kuja kumtetea Azpilicueta.

Baada ta tukio hilo, Spahic aliamriwa kutoka nje na mwamuzi wa mchezo huo.
Angalia video hii

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top