MOURINHO KUMPA RIO SHAVU JIPYA UNITED

Gazeti la Daily Mirror limeripoti kuwa kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho, anataka kumleta mchezaji wa zamani wa<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> klabu hiyo Rio Ferdinand na kumfanya kuwa kocha wake msaidizi.

Taarifa za awali zinadai kwamba Mreno huyo tayari ameshafanya hatua za awali ili kujihakikishia kama legend huyo wa Man United anaweza kurudi tena Old Trafford kwa kazi hiyo.

Kutokana na Ryan Giggs kukataa ofa ya kuwa kocha msaidizi chini Mourinho, Mreno huyo anataka kumleta Rio ili kuhakikisha kuwa anafanya kazi na mtu ambaye anaijua vizuri United ndani na nje.

Licha ya kumtaka Rio, Mourinho bado atamleta msaidizi wake wa muda mrefu Rui Faria lakini anaamini kufanya kazi na mtu anayejua vizuri United anahisi ni jambo lenye mantiki ili kumsaidia kujenga mahusiano mazuri na mashabiki.

Rio anaonekana kuwa mtu sahihi

Kutokana na historia kubwa aliyonayo katika klabu ya United ikiwemo kutwaa ndoo 12 kwa kipindi chote alichodumu na klabu, Rio anaonekana kuwa mtu sahihi wa kushika nafasi hiyo hasa kutokana na heshima kubwa aliyonayo kwa mashabiki. Kwa sasa Rio ni mchambuzi wa masuala ya soka.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top