Upinzani waandamana tena Kenya

Muungano huo unasema tume ya sasa ya uchaguzi haiwezi kuandaa uchaguzi huru

Muungano wa upinzani nchini Kenya CORD unafanya maandamano katika miji mikuu nchini humo kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Taifa ya Uchaguzi (IEBC) kujiuzulu.

Viongozi wa muungano huo wamesema maafisa hao hawawezi kuandaa uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na marungu kutawanya maandamano sawa na hayo Jumatatu wiki iliyopita.

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu walisema polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano hayo.

Taarifa kutoka mji wa Mombasa zinasema polisi tayari wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.nMashirika ya haki za kibinadamu yanasema polisi walitumia nguvu kupita kiasi wiki iliyopita

Mtu aliyeshuhudia amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema polisi wa kukabiliana na fujo wamekuwa wakishika doria katika barabara za mji huo.

Maduka mengi yamefungwa kutokana na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo na kutokea kwa uporaji.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top