TAARIFA KWA UMMA 17/5/2016: KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU CHINI


Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wakazi wa jiji la Dar-es-salaam pamoja na Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 10 kuanzia saa 5 asubuhi Jumanne, Tarehe 17/05/2016.
Sababu za kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Chini ni kuzuia uvujaji uliotokea mtamboni kwenye bomba la inchi 72. Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo katika Jiji la Dar es salaam kukosa Maji:
MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.
DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 
022-2194800 au 0800110064 (BURE)


IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

DAWASCO-MAKAO MAKUU





Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top