Makandarasi Jipangeni Mtumie Fursa Kwenye Miradi- Prof Mbarawa

Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka makandarasi pamoja na wadau wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>ujenzi nchini kuhakikisha wanajipanga kutumia fursa zitakazotolewa na serikali ambayo itatoa kipaumbele kwa makandarasi wazalendo katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

Amesema zipo fursa nyingi za ndani na nje ya nchi kwa makandarasi na wadau katika sekta ya ujenzi, kufuatia nia ya serikali ya awamu ya tano kutaka kuibadili Tanzania kuwa nchi ya viwanda vikiwemo vikubwa, vya kati na vidogo hivyo ni vyema wakajipanga kutumia fursa hiyo kubwa ili kujijengea uwezo na kujiendeleza kiuchumi,

Akizungumza kwenye mkutano wa mashauriano ya makandarasi na wadau wa ujenzi jijini Dar es Salaam Profesa Mbarawa amesema serikali kwa upande wake inajipanga kuanzisha miradi maalum kwa ajili ya kuwajengea uwezo makandarasi wazalendo kama alivyoagiza Rais Dk John Magufuli.

Profesa Mbarawa amesema kiasi cha asilimia 46 ya fedha zote za maendeleo sawa na shilingi Trilioni 4.6 zimepelekwa kwenye wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano kwa mara ya kwanza kutokea, ikionyesha nia ya dhati ya serikali kutoa kipaumbele kwenye ujenzi wa miundombinu nchini.

Mwenyekiti wa bodi ya usajili ya makandarasi CRB, Injinia Consolatha Ngimbwa, amesema katika mkutano huo wa siku mbili wamefikia maazimio kadhaa ikiwemo kuiomba serikali kutenga miradi mikubwa maalum kwa ajili ya kukuza uwezo wa makandarasi wazalendo na kwamba makandarasi watakaopewa kazi hizo kuzingatia weledi na maadili kufanikisha malengo ya mradi, huke kwa wale watakaokiuka mikataba bodi ya usajili ya makandarasi iwachukulie hatua kali za kisheria.

Katika Mkutano huo uliobeba kauli mbiu isemayo juhudi za makusudi za kukuza uwezo wa makandarasi wazalendo kwa maendeleo ya kiuchumi endelevu; changamoto na mustakabali wake, Waziri wa ujenzi pia alipata fursa ya kutoa vyeti kwa washiriki wa mkutano huo.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top