Majaji na mahakimu nchini wametakiwa kutoa nakala za hukumu mapema kwa wateja wao ili waendelee kuwa na <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>imani na mahakama hizo hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Jaji Mkuu Mohammed Othman Chande alipozungumza na mahakimu wa mahakama zote wa Mkoa wa Geita mjini Geita wakati akishauriana nao juu ya utoaji wa haki kwa wateja wao, ambapo amesema ni wajibu wa majaji na mahakimu kujenga imani ya wananchi kwa mahakama hususan pale wanapotia nakala ya hukumu mapema bila wananchi kuzungushwa.
Awali mahakimu hao kupitia hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Geita Ushindi Swallo walimwambia Jaji Mkuu kwamba kukosekana kwa vitendea kazi katika mahakama za mwanzo kunachangia kuchelewa kwa kesi.
Baadhi ya Wananchi waliokuwa katika viwanaja vya mahakama wametoa maoni yao juu ya uendeshwaji wa kesi katika Mkoa wa Geita.
Jaji huyo amefanya ziara yake ya siku moja na anaendelea kuzungukia baadhi ya Mikoa ya kanda ya ziwa lengo likiwa kushauri juu ya utoaji wa haki mapema kwa wananchi.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)