Zika: WHO laondoa wasiwasi katika Olimpiki

Mji wa Rio de Jeneiro
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa limeingilia kati katika kukabiliana na virusi vya Zika huku kukiwa na<endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
wito kwa mashindano ya michezo ya Olimpiki kuahirishwa kufuatia mlipuko wa virusi hivyo.

Afisa wa WHO Bruce Aylward ameiambia BBC kwamba hatua za kukabiliana na ugonjwa huo zimekamilishwa.Watoto walioathirika na Zika

Alikiri kwamba shirika la afya duniani WHO linaweza kufanya kazi nzuri zaidi kupitia kutoa tangazo kuhusu kile kinachoendelea na kwamba hakuna haja ya kuahirisha michezo hiyo.

Katika barua ya wazi wanasayansi 152 walisema kuwa utafiti waliofanya kuhusu Zika umeonyesha kuwa ni hatari kwa michezo hiyo kuendelea.Wanasayansi wataka mashindano ya Olimpiki kuahirishwa

Pia wamesema kuwa shirika hilo la afya duniani linafaa kufuata maelezo yake kuhusu Zika.

Ugonjwa huo unahusishwa na watoto walio na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa.Maafisa wa afya wakabiliana na Zika

Kati ya Februari na Aprili,Brazil ilisajili zaidi ya visa 90,000 vya Zika.

Visa vya watoto waliohusishwa na virusi hivyo ni 4,908 kufikia mwezi Aprili.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top