Trump alipa dola milioni 25 kumaliza kesi


Wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji 
  Wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji

Wakili wa rais mteule wa Marekani Donald Trump ametatua kesi ya mamilioni ya madola iliyokuwa inamkabili mteja wake ili apate nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya na kuangazia changamoto zinazoikabili Marekani.

Trump alikuwa ameshtakiwa na wanafunzi wa zamani kwa ubadhirifu wa pesa katika chuo kikuu cha Trump,ambapo wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji

Rais huyo mteule amekuwa akikanusha madai hayo lakini hatimaye ameamua kulipa dola milioni ishirini na tano ili kumaliza kesi hiyo. Mpango huo hata hivyo haumuhitaji kukiri kwamba alifanya makosa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top