African Lyon imekuwa timu ya kwanza kuifunga Simba SC tangu kuanAza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2016/17.
Bao pekee la Abdulla Msuhi limeifanya
Simba kuangusha pointi tatu kwa mara ya kwanza msimu huu wakati raundi ya kwanza ikielekea ukingoni.
Awali Simba ilikuwa haijapoteza mchezo hata mmoja kati ya michezo 13 iliyokuwa imecheza, imejikuta ikiangukia mikononi mwa Lyon katika mchezo wake wa 14 na kubakiza mchezo mmoja kukamilisha duru la kwanza la ligi msimu huu.
Simba iliiingia uwanjani ikiwa na pointi 35 kileleni mwa ligi pointi 21 zaidi ya Lyon ambayo ilikuwa nafasi ya 11 kabla ya mchezo wa leo.
Ushindi wa leo kwa Lyon ni faraja ambapo ilikuwa imecheza michezo 6 ya nyuma na kushinda mchezo mmoja pekee, hivyo ushindi dhidi ya Simba ni ushindi wao wa pili katika mechi zao 7 za hivi karibuni.
Dondoo
Simba imeruhusu goli kwa mara ya kwanza tangu iliporuhusu goli kwenye mchezo dhidi ya Yanga October Mosi.
Lyon imeshinda mechi ya pili katika mechi zake saba za hivi karibuni. Ushindi mwingine ulikuwa dhidi ya Mbeya City (22/10/2016 African Lyon 2-0 Mbeya City), katika mechi hizo imepoteza mechi tatu (12/10/2016 Mwadui 2-0 African Lyon, 19/10/2016 African Lyon 0-2 Majimaj,i 02/11/2016 Ruvu Shooting 1-0 African Lyon) na kutoka sare katika mechi mbili (15/10/2016 Stand United 1-1 African Lyon, African Lyon 1-1 Tanzania Prisons).
African Lyon vs Simba head to head
African Lyon imeshinda kwa mara ya kwanza dhidi ya Simba katika mechi 7 za ligi walizokutana, mechi 6 zilizopita Simba ilishinda zote.
06/11/16 African Lyon 1-0 Simba
26/01/13 African Lyon 1-3 Simba
15/09/12 Simba 3-0 African Lyon
31/03/12 African Lyon 0-2 Simba
16/10/11 Simba 4-0 African Lyon
03/02/11 African Lyon 0-3 Simba
21/08/10 Simba 2-0 Lyon
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)