Makonda azidi kuwabana wenyeviti wa Mitaa, Amburuza mwingine rumande


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana aliliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Zavala kata ya Buyuni Ilala, Chiku Said baada ya kutuhumiwa kuuza viwanja vya watu pamoja na serikali kinyume na sheria.


Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kuuza viwanja vya serikali kinyume na sheria bila kuwahusisha wajumbe wenzake hali ambayo imesababisha mgogoro mkubwa wa ardhi katika eneo hilo


Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa kumtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela kuthibitishwa kuuzwa kwa eneo hilo kinyume na sheria.


“Mkuu wa mkoa, ni kweli tulikuwa na eneo Block J lakini limeuzwa,” alisema afisa huyo “Nataka kuwaambia kitu wenyeviti wa mtaa hawaruhusiwi kuuza eneo katika mtaa. Mimi ningewataka wenyekiti kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kuepuka kutokea kwa hayo mambo,”


Baada ya kauli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Makonda akaliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top