Lowassa aeleza kwanini hakuhudhuria misiba ya Samwel Sitta na Mungai



Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoonekana kwenye misiba ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na waziri wa Elimu
wa zamani, Joseph Mungai.


Sitta alifariki Novemba 7 mwaka huu nchini Ujerumani alipokuwa ameenda kutibiwa maradhi ya tezi dume ambapo siku iliyofuata alifariki Mungai.


Lowassa amesema kuwa hakuweza kuhudhuria kwakuwa alikuwa nchini Afrika Kusini akimuuguza mdogo wake, Bahati Lowassa.


“Mdogo wangu Bahati Lowassa ni ofisa ubalozi nchini Afrika Kusini, alikuwa anaumwa na alikuwa amelazwa. Kwa siku zote nilikuwa huko kumuangalia. Nisingeacha kuhudhuria misiba hiyo,” Lowassa

Mwanasiasa huyo ameongeza kuwa alikuwa pamoja na waombolezaji kwa kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sitta kupitia vyombo vya habari pamoja na kumtumia mwanasheria wake kuwasilisha salamu zake za rambirambi kwa familia ya Mungai.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top