Taifa Stars yazawadiwa milioni 21 na ushee, Nigeria

Tanzania
Taifa Stars wakipiga jaramba

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za shukrani kwa Gavana wa Jimbo la Akwa Ibom, Gabriel Emmanuel kwa zawadi ya dola 10,000 za Marekani (sawa na Sh milioni 21.5) kwa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania 'Taifa Stars' baada ya kuonesha mchezo mzuri na wa upinzani dhidi ya wenyeji Super Eagles ya Nigeria uliofanyika Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabo, mjini Uyo.

Taifa Stars ilicheza mechi hiyo Jumamosi Septemba 3, 2016 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 mara baada ya kuibana Super Eagles hivyo kumsukuma Gavana huyo kuandaa hafla ya chakula cha jioni ambako mbali ya kuizawadia Stars, pia aliizawadia Super Eagles dola 35,000 za Marekani.

Taifa Stars ilitua Dar es Salaam usiku wa kuamkiia leo Septemba 5, 2016 ambako baadhi ya wachezaji walipelekwa Hoteli ya Urban Rose, iliyoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakati wengine hususani wale wa timu ya Azam FC walichukuliwa na viongozi wao kwa ajili ya safari ya kwenda Mbeya ambako Jumatano wanatarajiwa kucheza na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Sokoine mjini humo.

Wakati nyota 18 wakitua Dar es Salaam, Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta aliishia Nairobi, Kenya ambako aliunganisha ndege ya kwenda Brussels, Ubelgiji.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top