Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Amteua Bw. Waziri Waziri Kindamba Kuchukua Nafasi Hiyo




Kufuatia hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na hivyo Serikali
kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.


Bw. Waziri Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo tarehe 23 Septemba, 2016.


Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


23 Septemba, 2016
Habari zilizopo katika magazeti ya leo ijumaa september 23, 2016 bofya hapa
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top