Mwl Joseph b Maduka.
🔹Pindi watu wa imani /madhehebu tofaut wanapotaka kufunga ndoa kuna changamoto kadhaa zinaweza kujitokeza
🔹 Ingawa wote tunasema ni wakristo na tunatumia Biblia moja lakini ki Ukweli kuna tofautI kubwa sana kati yetu.
🔹Tofauti hizi ndizo zinazoleta mkanganyiko mkubwa Katika jamii, hivyo nitaenda kuongelea baadhi ya changamoto hizo kwa wanandoa watarajiwa walio madhehebu tofauti.
1. UTOFAUTI WA KIMAPOKEO.
🔹Kikwazo cha kwanza ambacho wachumba walio madhehebu tofauti watakutana nacho ni utofauti wa kimapokeo Katika dini zao.
🔹Malezi tunayoyapata Katika familia zetu na makanisa yetu yana mchango mkubwa sana Katika kesho yetu. Mfano binti ni mpentekoste na kijana wa kiume msabato.. Hawa wamelelewa Katika Malezi tofauti mpaka wanafika umri wa kujitegemea.
🔹Sasa inapotokea kijana anamuambia binti inabidi uache kwenda kanisani jumapili na uwe unaenda jumamosi maana ndio siku ambayo Bwana ameichagua, usidhani kuwa itakuwa rahisi.
🔹Au Kijana ni mpentekoste halafu binti ni mkatoliki, unafikiri itakuwaje?? Huyu anaamini ubatizo wa watoto na ubatizo wa maji machache wakati mwingine anasema watoto hawabatizwi na ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (kuzamishwa mwili mzima).. Hapo upinzani utakuwa ni sawa Israeli na Palestina kila upande unajiona una HAKI na upo Sahihi.
🔹Pasipo kukubaliana, mmoja kukubali kumfuata mwenzake basi safari itahairishwa njiani. 👇
"Je watu Wawili, waweza kutembea pamoja Wasipokuwa WAMEPATANA..? "
Amosi 3 :3
2. UPINZANI TOKA KWA WAZAZI.
🔹Kama Wakifanikiwa kuvuka Kikwazo cha kwanza ambacho ni makubaliano yao wenyewe, Kikwazo cha pili watakachokutana nacho ni familia zao.
🔹Wazazi wana nafasi kubwa Sana Katika Maamuzi ya Ndoa ya Watoto wao na ndoa inatakiwa ipate Baraka kutoka familia za pande zote mbili (familia ya upande wa mwanamke na familia ya upande wa mwanaume).
🔹Kama imetokea moja ya familia ikawa kinyume na hiyo ndoa, basi tayar ndoa hiyo imeshaingia Kasoro.
🔹Sasa kuna baadhi ya familia wamejikita kwenye dini kiasi kwamba wapo tayari hata KUFA kusimamia dini zao, Inapotokea binti /kijana wao anatakiwa aoe/kuolewa na mtu wa imani tofauti wapo tayar hata kutamka LAANA na wengine KUWATENGA kabisa watoto wao.
🔹Jambo hili huwa linanishangaza sana, Katika maajabu ya Ukristo hili nalo ni moja wapo. Mzazi kumkataa Mtoto kwa ajili ya kutetea misimamo yake na heshima yake, hii si Sawa. Anyway..! Nitaongea kitu hapo mwishoni.
🔹Changamoto hii ni kubwa na ndogo sana inategema na msimamo na Hekima ya familia husika. Hivyo kama kijana unataka kuoa /kuolewa na mtu wa dhehebu tofaut basi unatakiwa kujiandaa kwa changamoto hii.
3. WAPI NDOA ITAFUNGWA.
🔹Hii ni changamoto nyingine ambayo haikwepeki, ni lazima ndoa ifungwe Katika kanisa fulani, swali Je ni kanisa lipi? Kijana mpentekoste wakati binti ni msabato.
🔹Unaweza ukasema mwanamke anatakiwa kumfuata mwanaume hivyo ndoa ifungwe Pentekoste, Lakini JIBU si rahisi kiasi hicho.
🔹Watu wamekaa kuvutana Katika swali hili bila kupata muafaka, kila upande unavutia kwake. Ni Hekima tu ya Mungu ihusike hapa.
4. MALEZI YA WATOTO.
🔹Hiki ni kipengele cha mwisho kama vyote hivyo vya mwanzo vimepatiwa majibu. Baada ya sherehe ya ndoa maisha mapya yanaanza. Je mmejiandaaje kwa maisha hayo?
🔹Je ni wapi mtaabudu? Mtaabudu sehemu moja au kila mtu atasali kwake? Na kama kila mtu atasali kwake, vipi watoto wataenda upande gani kwa baba au kwa mama?
🔹Ni vizuri ukiwa umejiandaa kwa changangamoto hii mapema kabla hamjaingia kwenye ndoa, kama mkisubiri mpange mkishaingia mtakuwa Mmechelewa, na malumbano yanaweza yakaibuka yasiyo kuwa na ulazima kama mambo haya yangejadiliwa MAPEMA.
.......................
USHAURI WANGU :
👉KWA VIJANA : kama imetokea unataka kufunga ndoa na mtu wa dhehebu tofauti, basi unapaswa kufahamu changamoto zilizopo Katika UAMUZI unataka kuchukua,Ujiandae kukabiliana nazo na ZAIDI Uombe Mungu akusaidie Uvuke Katika changamoto hizo.
👉KWA WAZAZI : Wazazi wanatakiwa kuwa FARAJA na MSAADA mkubwa kwa watoto wao pindi wafikapo Katika hatua hiyo muhimu, na si kuwa KIKWAZO cha kuwazuia watoto wao kufanikisha MALENGO yao.
PIA WANATAKIWA KUTETEA WOKOVU NA SI KUTETEA DINI ZAO. KWANI HAKUNA ATAYEINGIA MBINGUNI KWA AJILI YA DINI.
👉KWA VIONGOZI WA KIROHO : Wanapaswa kufundisha KWELI ya MUNGU na si MAPOKEO ya Dini zao, Waache Kutengeneza MATABAKA Katika IMANI, Pia Waache kuwaaminisha WASHIRIKA wao kuwa wao ni BORA kuliko Wakristo wa madhaehebu Mengine.
Watumishi wamechanganya Sana kanisa kwa Uchu wao wa heshima, Madaraka na tamaa zao binafsi, na wakristo wamekuwa WAHANGA wasio na MATUAMAINI kutokana na Vitendo vyao.
ANGALIZO.
UJUMBE HUU UNAZUNGUMZIA UTOFAUTI KATI YA WACHUMBA WALIO KATIKA MADHEHEBU YA KIKRISTO NA SI MKRISTO NA MTU WA IMANI NYINGINE.
BILA KUSAHAU NDOA YA MTU ALIYEOKOKA NA ASIYEOKOKA NI KINYUME NA NENO LA MUNGU NA HAIRUHUSIWI BILA KUJALI DHEHEBU.
KUMBU 7:2, 2 WAKORINTHO 6 :14 - 18.
♥NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE
WAEBARANIA 13 :4

Nafasi zaidi za kazi bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)