Wales 3-0 Urusi

Aaron Ramsey
Wales ilijifurukuta na kuilaza Urusi mabao matatu kwa nunge katika mechi ya mwisho na muhimu ya makundi jana usiku.

Aaron Ramsey na Neil Taylor na Gareth Bale walifunga mabao hayo muhimu na kuisaidia timu hiyo ya kocha Chris Coleman ikiwa imejihakikishia nafasi katika mkumbo wa pili kwa mara ya pili katika historia yake.Wales 3-0 Urusi

Wapinzani wao wa jadi England walimudu sare tasa dhidi ya Slovakia mjini Saint-Etienne na kuhakikisha kuwa Wales wanafuzu kwa raundi ya pili ya mashindano hayo kama vinara wa kundi B.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Wales sasa watachuana na mshindi wa tatu katika kundi C A ama D.Aaron Ramsey na Gareth Bale

Wales na England zimefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Euro baada ya mechi zake za kundi B kukamilika.

Vijana wa Chris Coleman wamewabamiza Russia mabao 3 kwa 0 na huku England ikija ya pili kwenye kundi baada ya kubanwa mbavu na Slovakia.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top