Jonathan afanyiwa uchunguzi unaohusu ufisadi

Goodluck Jonathan
Aliyekuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema kuwa amefanyiwa uchunguzi unaohusu ufisadi uliofanywa na serikali ya mrithi wake Muhammadu Buhari,

Hata hivyo alikataa kusema kile ambaho uchunguzi huo utafichua, akisema anaiacha serikali ya Buhari kufanya kazi yake.

Buhari amewalaumu maafisa wa serikali ya zamani kwa kupora mabilioni ya dola, lakini bwana Jonathan anasema kuwa utawala wake ulifanya mengi kupambana na ufisadi.Muhammadu Buhari

Jonathan alikana madai kuwa akiba za serikali zilikuwa tupu wakati aliondoka ofisini mwaka uliopita.

Jonathan ndiye rais wa kwanza kusalimisha madaraka baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top