Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko
Waziri wa Michezo wa Urusi, ameomba msamaha, kwa kashfa iliyohusu madawa ya kusisimua misuli kutumiwa kwenye michezo , kashfa ambayo inaweza kupelekea wanariadha wa Urusi kupigwa marufuku kushiriki kwenye Olimpiki nchini Brazil mwaka huu.
Katika makala yake kwenye gazeti la Uingereza, The Sunday Times, waziri huyo wa Urusi, Vitaly Mutko, alisema makosa makubwa yamefanywa, na kashfa imeitia aibu Urusi. Lakini Bwana Mutko hakusema kama serikali ilihusika.Kashfa inaweza kupelekea wanariadha wa Urusi kupigwa marufuku kushiriki kwenye Olimpiki
Juma lilopita, afisa wa Urusi, wa kupambana na madawa kutumiwa kwenye michezo, Grigoriy Rodchenkov, alisema kuwa kulikuwa na mpango wa kufanya udanganyifu katika Olimpiki za majira ya baridi, zilizofanywa Sochi, miaka miwili iliyopita, na kwamba serikali iliunga mkono mpango huo.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)