Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi, I’m Sorry JK umefungiwa.
Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA Jumatano hii kujielezea kuhusiana na wimbo huo. Kupitia Instagram, Nikki amewaonya watu dhidi ya kuusambaza wimbo huo kwakuwa mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye Instagram.
“Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili,” ameongeza.
Pia ameonya, “Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.”
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook: Serikali imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki Mbishi. Wallah nilidhani ni utani kumbe Kweli? Serikali hii inachoogopa ni nini? Dah kua uyaone.”

Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)