Rais wa Uturuki Awasili Nchini Kwa Ziara ya Kikazi


RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini jana jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.


Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak


Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan aliyefuatana na mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top