Watoto kuzaliwa na wazazi watatu Uingereza

Mtoto

Serikali nchini Uingereza imeidhinisha shughuli ya kimatibabu ambayo itawezesha watoto kuzaliwa na wanawake wawili na mwanamume mmoja.

Uamuzi huo wa kihistoria unatokana na uvumbuzi wa kisayansi ambao unalenga kuzuia watoto kuzaliwa wakiwa hawana matatizo ya kurithi kutoka kwa wazazi hao.

Madaktari Newcastle - waliovumbua aina hiyo mpya ya IVF (njia ya kutungishia mayai mbegu nje ya mama na kuyarejesha katika mji wa uzazji) - wanatarajiwa kuwa wa kwanza kutoa huduma hiyo kwa na tayari wametoa wito kwa watu wanaotaka kutoa mayai kujitokeza.

Mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa njia hiyo anatarajiwa mwishoni mwa mwaka 2017.

Baadhi ya familia zimewapoteza watoto kadha kutokana na matatizo yasiyoweza kutibiwa, ya cha chembe zilizo ndani ya seli ambazo hufahamika kama mitochondria, yanayotokana na chembe za kinasaba au jeni. Baadhi ya matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwaacha watu wakiwa hawana nguvu ya kuufanya moyo kuendelea kupiga na hivyo kufariki.
Msichana anayetarajia 'kufufuka' kuhifadhiwa
Mwanamke ajifungua kwa kutumia tishu za ovari za utotoni

Magonjwa haya huendezwa kutoka kwa mama pekee na kwa hivyo njia ambayo inawezesha kutumiwa kwa yai kutoka kwa mtu mwingine kwa kuchanganya na yai la mama na kisha kuongeza mbegu za baba inaweza kusuluhisha tatizo hili.

Ni njia hii ambayo inawezesha mtoto kuwa na mama wawili wazazi, kibiolojia, na baba.

SMtoto anayezaliwa anakuwa na sehemu fulani ya DNA kutoka kwa aliyetoa yai.

Shughuli hiyo ya kimatibabu inakubaliwa sasa kisheria, kimaadili na kila kitu kiko tayari kuifanikisha kisayansi.

'Uamuzi wa kihistoria'

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Utungishaji Mbegu miongoni mwa Binadamu (HFEA) Sally Cheshire amesema: "Ni uamuzi wa umuhimu mkubwa. Ni uamuzi unaohusu kusonga mbele kwa makini na si kusonga tu, bado kuna safari ndefu."

"Nina uhakika wagonjwa watafurahia sana uamuzi huu wa leo."

Lakini baadhi ya wanasayansi wamekosoa njia hii wakisema itafungua mlango kwa watu kutaka kujifungua watoto wa 'mitindo' ambapo watataka kuwa na watoto wa jeni wanazozitaka.
Binadamu mzee zaidi asherehekea siku ya kuzaliwa
Huenda watoto wakazaliwa bila wanawake

Kabla ya njia hii mpya ya uzazi kutumiwa, HFEA itahitajika kutoa idhini kwanza.

Watoto wa wazazi watatu watakubaliwa tu katika hali ambapo hatari ya mtoto kupata maradhi ya mitochondrial iko juu.

Kliniki na vituo vya afya sasa vinaweza kuwasilisha maombi kwa HFEA kupata leseni ya kufanikisha uzazi wa IVF wa kutumia watu watatu.
Sharon Bernardi na mwanawe Edward, aliyefariki mwaka jana akiwa na miaka 21
Sharon Bernardi na mwanawe Edward, aliyefariki mwaka jana akiwa na miaka 21. Sharon amewapoteza watoto wake wote saba kutokana na matatizo ya mitochondria.
Hufanya kazi vipi?

Maradhi ya mitochondrial husababishwa na kasoro kwenye mitochondria - chembe ndogo ndani ya seli ambazo hubadilisha chakula kuwa kawi inayoweza kutumiwa na mwili.

Mmoja kati ya watoto 4,300 huzaliwa na tatizo hili. Dalili huwa misuli isiyo na nguvu, upofu, kutoweza kusikia, kifafa, matatizo katika kujifunza mambo, kisukari na matatizo ya moyo na ini.

Wengi hufariki.

Lengo la njia hii ni kuchukua mitochondria isiyo na kasoro kutoka kwa mwanamke mwingine.

Lakini mitochondria huwa na DNA yake, jambo ambalo litasababisha watoto watakaozaliwa na DNA kutoka kwa watu watatu.

Hata hivyo, DNA zinazoamua sifa za mtu kimwili na kitambia zitatoka kwa wazazi kamili.
Wa kwanza duniani?

Uingereza hata hivyo haitakuwa nchi ya kwanza kuwa na watoto waliozaliwa kupitia njia hii ya kuwa na wazazi watatu.

Familia moja kutoka Jordan ilisaidiwa na madaktari kutoka New York kutumia njia hiyo nchini Mexico na mtoto aliyezaliwa kwa njia hiyo anaaminika kuwa buheri wa afya.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top