Uhamiaji Yazipiga Marufuku Simba, Yanga na Azam Kutumia Wachezaji wa Kigeni



Serikali imevipiga marufuku Klabu za ligi kuu Tanzania hususani Simba, Yanga na Azam kuwatumia wachezaji wa kigeni mpaka watakapokamilisha taratibu zao za uhamiaji.

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya klabu ya Ndanda FC kutuma malalamiko TFF kwamba Simba iliwatumia wachezaji wake wawili wa kigeni Daniel Agyei na James Kotei kwa madai kwamba hawana vibali vya kufanya kazi nchini.

Klabu hizo zimepewa maagizo kwamba wachezaji na makocha wote wa kigeni ambao hawajakamilisha taratibu za uhamiaji hawatoruhusiwa kuzihudumia klabu zao hadi hapo watakapokamilisha taratibu hizo.

Idara ya uhamiaji kupitia kwa afisa uhamiaji John Msumule leo alitoa tamko kwa klabu zote za Ligi Kuu Tanzania bara kutoendelea kuwatumia wachezaji wake wa kigeni hadi watakapotimiza masharti ya uwepo wao nchini kisheria na uhamiaji wamezitaka klabu za Simba, Yanga na Azam FC kuhakikisha wachezaji wake na makocha wao wa kigeni wanapata vibali vya kufanyia kazi nchini pamoja na kuishi.

Hata hivyo kwa upande wa Yanga wao wachezaji wao wana vibali vya kazi na vya kuishi nchini isipokuwa makocha wao ndio wana vibali vya kazi pekee.

Kwa upande wa watani zao wa jadi Simba wao hawajatimiza vigezo hivyo kwa wachezaji wao wa kigeni na makocha wao, hivyo hawaruhusiwi kuendelea kuwatumia wachezaji wao ambao hawana vibali mpaka watakapo vipata vibali ingawa uongozi wa klabu ya Simba ulisema kuwa wachezaji hao wamekamilika kila kitu.

1 maoni:

Sasa TFF ni waongo! Simba apokonywe ushindi na kupewa Ndanda!

Reply

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top