Serikali ya Nigeria Yakamata magunia 102 ya 'Mchele wa Plastiki'


Mara nyingi tumekuwa tukisikia juu ya vipodozi bandia au dawa bandia lakini masuala yanayohusu chakula bandia hayakuwa yakigonga vichwa vya habari sana hadi hivi karibuni dunia ilipopata mshtuko juu ya uwepo wa mchele wa bandia.


Mchele huu wa bandia ambao umekuwa ukihatarisha afya za watu wengi hufanana sana na mchele wa kawaida kiasi kwamba ukiiangalia kwa macho huwezi kuutofautisha.

Mchele huu unaosambaa kwa kasi duniani hutengenezwa kwa plastiki na utofauti wake na mchele wa asili huonekana mara baada ya kuupika.


Jana, mamlaka katika mji wa Lagos nchini Nigeria ilikamata magunia 102 ya mchele wa plastiki yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sikukuu ili kujipatia fedha nyingi zaidi.

Nigeria inaendelea na uchunguzi kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria


Mchele huu umeelezwa kuwa ni hatari sana kwa afya ya binadamu kwani ni sawa na kumlisha mtu plastiki lakini pia wingi wa kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa mchele huo.


China imedaiwa kuwa ndiyo nchini inayoongoza kwa utengenezaji wa mchele huu.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top