Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu wawili wa JWTZ kuwa Meja Jenerali kuanzia tarehe 03 Disemba 2016. Maafisa Wakuu hao ni;
Brigedia Jenerali George William Ingram ambaye ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga, na Brigedia Jenerali Michael Wambura Isamuhyo ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu anawapongeza na kuwatakia kheri katika vyeo vyao vipya.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na
Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638/0756-716085R5
Brigedia Jenerali George William Ingram ambaye ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga
Brigedia Jenerali Michael Wambura Isamuhyo ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)