Mchungaji Awanywesha waumini dawa ya kuua bakteria “Dettol” ili Wapone Matatizo Yao


Mchungaji maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashangaza watu kwa kitendo cha kuwanywesha Dettol waumini wake ilihali ina madhara kwa binadamu.


Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.


“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,” – Mchungaji.


Pia alisema kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa


“Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa ya Oxygen mwilini. Hali hiyo ikitokea mtu anaweza kupoteza fahamu na kufariki.

“Na kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua”


Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata..

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top