Ban Ki-moon Anataka Kugombea Urais Nchini Korea Ya Kusini




Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amedokeza kuwa huenda akawania urais nchini mwake, Korea Kusini.


Muhula wake Ban kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa unakamilika mwisho wa mwezi huu wa Disemba. Wakati wa mkutano wake wa mwisho
na waandishi wa habari, Ban alisema kuwa baada ya kupata mapumziko anarudi nchini mwake Korea Kusini kuona vile ataisaidia nchi yake.
Uchaguzi wa uraia nchini Korea Kusini unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka 2017.


Lakini huenda uchaguzi huo ukafanyika katika muda wa miezi miwili baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura ya kumuondoa madarakani Rais Park Geun-hye, kutokana na sakata, ambapo analaumiwa kwa kumruhusu rafiki wake wa karibu kunufaika kifedha.


Ikiwa mahakama ya katiba itadumisha kura hiyo ya kumuondoa, atakuwa rais wa kwanza wa Korea Kusini aliye madarakani kuondelwa katika kipindi cha uhuru wa nchi hiyo. Mahakama ya katiba ina siku 180 kutoa uamuzi wa mwisho. Matamshi ya Ban yanakuja huku yakishuhudiwa maandamano kwenye mji mkuu wa Korea Kusini, Seol.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top