VIJANA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KAMBI YA JKT KANEMBWA AWAMU YA PILI


TAARIFA KWA UMMA


1. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawatangazia vijana wa Kitanzania wito wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu
ya pili na Vijana wa Kujitolea.


2. Vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo ni kama ifuatavyo:-


a. Vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli Awamu ya Pili.

Kundi hili linahusisha wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa kwenye mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga vyuo vya elimu ya juu.


b. Vijana wa Kujitolea

Kundi hili linahusisha Vijana wote waliosailiwa mwezi Mei na Juni mwaka 2016 katika ngazi za wilaya na mkoa na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.

3. Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na Kujitolea wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa wakiwa na vifaa vifuatavyo:

a. Bukta ya rangi ya bluu iliyokoza (Dark blue) yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma isiyo na zipu, iwe na urefu unaoishia magotini.


b. Raba ngumu za michezo zenye rangi ya kijani au nyeusi.


c. Shuka jozi mbili za kulalia zenye rangi ya bluu bahari ukubwa wa 4x6.

d. Soksi za michezo jozi mbili rangi nyeusi.


e. Chandarua moja ya duara rangi ya bluu au kijani ukubwa wa 4x6.


f. Nguo za michezo (truck suit) jozi moja rangi ya kijani au bluu.


g. Fulana (T-shirt) ya kijani isiyokuwa na maandishi yoyote.


h. Mavazi hayo yasiwe ya kubana mwili.


4. Inasisitizwa kuwa vijana wa kujitolea wanaotakiwa kuripoti makambini ni wale tu waliopita katika usaili kwenye ngazi

za wilaya na mikoa na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.


5. Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na Kujitolea wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia

tarehe 01 mpaka 05 Desemba 2016 kwa kujitegemea nauli ya kwenda na kurudi.







Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top