KISABABISHI CHA UMASIKINI TANZANIA NI ZAIDI YA VIONGOZI, UFISADI, NA UOZO WA VYAMA VYA SIASA



Na John S.M Mgejwa

Chanzo cha umasikini Tanzania ni kitu special kilicho ndani ya akili za watanzania ambacho kinazidi ufisadi na rushwa na uozo wa vyama vya siasa
.

Tunafahamu fika kwamba viongozi wana kazi ya ziada ambayo walitwishwa na wananchi wao kusimamia rasilimali zote za taifa, lakini hali imekuwa tofauti kwa Tanzania ingawa dunia inaamini hivyo kuwa usimamiaji mzuri wa rasilimali na utoaji fursa kwa wananchi ndiyo njia madhubuti ya kuleta maendeleo.

Ifike mahali watanzania tushtuke kwamba kuna kitu ambacho kiko juu ya hayo yanayoaminiwa duniani kuwa ndiyo chanzo cha maendeleo. Kwa muktadha huo ukiwa kama mtu unayehangaisha akili yako kufikiri kila kukicha katika hali ya sasa hutakiwi kabisa kulaumu kiongozi kwamba ndo anasababisha wewe uwe masikini. Nina sababu zifuatazo zinazoonyesha kuwa watanzania tunaendelea kuwa masikini kwa sababu ya kitu ambacho kipo ndani ya akili zetu ambacho kimewashinda viongozi kukisimamia maana mtanzania wa kawaida ukiwa "complex" katika kusimamiwa na kukupa siri za ushindi basi kwako kiongozi hatakuwa na maana hivyo hali itabaki kama ilivyo kila kukicha.

1. Mtanzania ana uwezo wa kumiliki iPad ya sh.1,000,000, simu ya laki 400, 000/ , 250,000 etc lakini bado anao uwezo wa kulaumu na kulalamika kuwa hana mtaji sasa hivi angekuwa mbali, hili tatizo linasababishwa na kile kitu special ambacho kimo ndani ya akili yake ambacho hata awe kiongozi wa namna gani hawezi kumletea maendeleo hadi pale mtanzania huyu atakapoondoa hicho kitu special ndani ya akili yake.
2. Mtanzania anauwezo wa kuunga bundle la 1000, 2000, kwa kwa siku , zidisha kwa siku thelathini alafu uzidishe kwa siku mia tatu sitini na tano (mwaka mzima) lakini bado anao uwezo wa kulalamikia viongozi wake eti hana kitu na maisha ni magumu, huu ni ujinga ambao unatakiwa kukomeshwa na yeye mwenyewe siyo kiongozi tena
3. Mtanzania anao uwezo wa kukata tiketi ya kutoka mwanza hadi Dar es salaam kwenda kumsalimia Shangazi, kaka , baba Mdogo nk au wakati mwingine kwenda kuzurura tu na kulifahamu jiji ilhali hapo alipo hana kazi yoyote , wala afikirii kuwa hiyo nauli angeifanyia mambo ya kumwingizia kipato. Itifaki imezingatiwa kwa wale wa mwanza ila mtu anaweza kusafiri kwenda mkoa wowote

4. Mtanzania anao uwezo wa kuwa hewani kuanzia asubuhi hadi SAA nane usiku aki comment picha za warembo na za handsome boys kila siku huku akisubiri dona maskani liive atoboe then aendelee kuchati

5. Mtanzania anauwezo wa kuhakikisha leo anunue nguo gani na achubue vipi ngozi ili atokelee vizuri zaidi , hapa anatumia pesa siyo mawe lakini analia hana mtaji

6. mtanzania anauwezo wa kiakili kujiuliza namna gani ya kuongeza nguvu za kiume na kuwapata warembo lakini mtakosana sana ukimwambia hiyo nguvu aitumie kutafuta pesa. Asilimia kubwa ya watanzania wanawaza na kujadili namna ya kumfikisha mwanamke kileleni na wanawake nao wanatumia kiasi kidogo walicho nacho kutengeneza makalio ili ngono ishamili zaidi na ukitaka kugombana naye mwambie atafute pesa au hiyo pesa bora angeanzisha "firm" Fulani ili imwingizie kipato kuliko kuongeza ukubwa wa kalio

6. Wasomi wengi wanatoka vyuoni wakiwa wamekomaa katika ubinafsi na hii ni kutokana na mfumo unaotumika mashuleni wa kufanya mitihani kwa kila mmoja huku akificha kazi yake ili mwenzake asiibie, kumbe Hali hii huendelea kwa zaidi ya miaka 16 hali ambayo huwafanya wasomi wengi wa tz na kwingineko kushindwa kuhimili vishindo vya mtaani kwani mtaani wanastaili nyingine ya maisha ambayo huhusisha kusaidiana na kushirikiana hata kwa mipango, mpango wako ni mpango wangu ilimradi tupate maendeleo . kumbe utokapo chuoni unatakiwa uache tabia za ujibuji mitihani kwani zitakufanya uishi maisha ya usiri sana kwa kila unachofanya utakuwa peke yako.

7. Mtanzania yuko tayari kubagua kazi kisa yeye ni msomi_ hili siyo tatizo la viongozi ni lako, usomi utakuwa bure kama unafikiri kupata pesa ni elimu mjinga we we!!!

Ukiangalia mambo hayo yote yanakugusa wewe mwenyewe siyo mwanasiasa na mbaya zaidi yako kwenye akili yako ambapo solution yake hadi wewe mwenyewe ujishtukie kwnza. Lucky Dube alisema hivi "I can sit here and teach you every trick in the book but at the end of the day it is your life. Good things come to those who got out and made them happen, they don't come to those who wait." Tatizo uko nalo kwenye akili siyo ufisadi maana ufisadi pia unasababishwa na hilo tatizo lililo ndani ya akili ya huyo fisadi.

Imeandikwa na John SM Mgejwa (The Economist)

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top