WHO: Sukari inaongeza hatari ya unene kupita kiasi




Vinyaji vyenye sukari nyingi vinalaumiwa kwa kuchangia magonjwa hatari kama vili kisukari.


Shirika la afya Duniani, WHO, linasema kuwa utumiaji ulioenea wa sukari, unachangia
pakubwa tatizo linaloendelea kuongezeka la unene.

Shirika hilo la umoja wa mataifa zinaitaka serikali kutoza ushuru bidhaa zenye sukari ilil kupunguza ueneaji wa unene, ambao ni tishio la kiafya duniani kote.

Ripoti hiyo mpya inaeleza kuwa theluthi moja ya watu wazima duniani kote ni wanene na nusu bilioni walikuwa wanene kupita kiasi mnamo mwaka wa 2014.

Cha kutia wasiwasi hata Zaidi ni kwamba shirika la Afya duniani, WHO, linakadiria kuwa watoto milioni 42 walio chini ya umri wa miaka mitano walikuwa wanene kupita kiasi mwaka jana. Hilo ni ongezeko la takriban watoto milioni 11 katika kipindi cha miaka kumi na mitano. Karibu nusu ya watoto hao wanaishi katika bara Asia na asili mia 25 wanaishi barani Afrika.

WHO inasema vyakula visivyo na manufaa kiafya ndivyo vya kulaumiawa kwa ongezeko la visa vya ugonjwa wa kisukari, ambao watu wapatao milioni 422 wanaugua, na unachangia Zaidi ya vifo 1.5 kila mwaka. Shirika hilo linasema kuwa utumiaji wa bidhaa za sukari, ikiwa ni pamoja na vinywaji vilivyojaa suukari, unachangia mno katika ongezeko la unene wa kupita kiasi na ugonjwa wa kisukari ulimwenguni. 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top