Wizara ya usafirishaji Marekani imepiga marufuku simu ya aina ya Samsung Galaxy Note 7 katika safari zote za ndege ndani ya Marekani baada ya matukio karibu 100 ya simu hiyo kupata joto la kupita kiasi na mara
nyingine kulipuka.
Idara ya safari za anga -FAA- ya Marekani awali ilihimiza wasafiri kuzima simu hizo wakiwa ndani ya ndege, na kuziweka katika masanduku wakati wa safari. Lakini marufuku hii mpya inakataza hata simu zilizozimwa ndani ya ndege na itaanza kutekelezwa Jumamosi mchana kwa saa za Marekani.
Kampuni ya Korea Kusini inayotengeneza simu hiyo inasema inawasiliana na wenye simu hizo kuwaelekeza kuhusu marufuku hiyo. Kampuni hiyo ilitangaza Jumatatu kuwa inasimamisha kutengeneza simu ya Galaxy Note 7 baada ya simu hizo kushika joto na nyingine kulipuka.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)