Tambwe awapa somo washambuliaji bara


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amis Tambwe amesema siri ya kuendelea kutikisa nyavu katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila kushuka, ni kwa vile amekuwa hasikilizi maneno ya mashabiki uwanjani.

Alisema mchezaji yeyote kama anahitaji kufanikiwa na kufanya vizuri katika ligi hiyo hapa nchini hana budi kuziba masikio ya mashabiki na kufanya kile ambacho kimemleta katika timu vinginevyo ni rahisi kupotea.

Tambwe hivi karibuni aliifungia bao timu yake katika mchezo dhidi ya Simba, ingawa inadaiwa kabla ya kufunga aliushika kwa mkono mpira huo.

Akizungumza na gazeti hili, mchezaji huyo wa zamani wa Simba, alisema anawajua mashabiki wengi wa soka wamekuwa ni wazungumzaji, na kwamba kama angekuwa anawafuatisha angekuwa ameshuka kiwango.

“Siku zote ukitaka kufanikiwa katika Ligi ya Tanzania ni lazima upambane kweli na kuacha kusikiliza maneno ya mashabiki, kwani ukiwafuatisha utaanguka na kupotea kabisa,” alisema.

Tambwe tangu kujiunga na Simba msimu wa mwaka 2013 na msimu uliopita Yanga, amekuwa akizidi kuonesha ubora wake katika kufumania nyavu huku msimu uliopita akiibuka kuwa mfungaji bora.

Alisema amejipanga kuhakikisha anaendelea kufanya vizuri sio katika kuifunga Simba bali katika michezo yote.












Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top