Simba SC yatamba iko vizuri


Meneja wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’



MENEJA wa klabu ya Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amesema siri ya timu yao kufanya vizuri kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ni ubora wa kikosi walichokisajili pamoja na umoja
na mshikamano waliokuwa nao.

Simba ndiyo vinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20 huku ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata moja katika mechi nane ilizocheza msimu huu.

Akizungumza na gazeti hili juzi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City Mgosi, mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, alisema ubora waliokuwa nao msimu huu ni vigumu kuwazuia kwa sababu wamekamilika katika idara zote muhimu ambazo ndizo zinachangia wapate matokeo hayo mazuri.

“Ukweli wale wanaosubiri kuona tunapoteza watasubiri sana, Simba ya msimu huu ina mabadiliko makubwa kuanzia wachezaji wote waliosajiliwa unaweza kuona kila nafasi ina wachezaji watatu hadi wanne lakini hata benchi la ufundi nalo ni bora kuanzia kocha mkuu hadi msaidizi wake sioni sababu ya kushindwa kufanya vizuri,” alisema Mgosi.

Mkongwe huyo aliyestaafu soka mwanzoni mwa msimu huu na kukabidhiwa cheo hicho cha Umeneja alisema, pamoja na kasi waliyoanza nayo lakini mambo bado kwani malengo yao ni kuhakikisha wanaendelea na kasi hiyo na kuhakikisha wanarudisha furaha kwa mashabiki wao wote wanaoipenda Simba katika kipindi chote ambacho walikaa na majonzi kutokana na timu hiyo kufanya vibaya.

“Dhamira yetu ni kwanza kuhakikisha tunashinda ubingwa wa Ligi Kuu, ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa na pia kurudisha furaha kwa kila shabiki na Mwanachama wa Simba ambaye alipoteza furaha kipindi chote cha misimu mitatu ambacho timu ilikuwa haifanyi vizuri,” alisema Mgosi.

Simba chini ya kocha Joseph Omog, imeshinda mechi sita na kutoka sare mbili, matokeo ambayo yameonesha kuvunja rekodi ya timu hiyo kwa misimu mitatu iliyopita ambapo haikuwa ikianza na kasi hiyo.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top