Wizara
ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia ,wazee na watoto inawatangazia
wahitimu wote wa vyuo vikuu vya kada mbalimbali za afya wanaopaswa
kufanywa mafunzo ya utarajali yani ‘internship’
ambao ni madaktari wa
meno, wafamasia, wauguzi, wataalamu wa Radiolojia, wataalamu wa maabara
na wataalamu wa afya ya mazingira kwamba pamoja na kuwa walipaswa kuanza
mafunzo yao leo Oktoba 1, 2016 ambayo ilikuwa ni tarehe rasmi ya
kuanza mafunzo hayo itatangazwa hapo baadae. Wizara ya Afya imesema kuwa kuchelewa huko ni kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na Wizara ili kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanaanza katika namna na mfumo uliobora zaidi.
Aidha Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammad bakari kambi (Pichani juu) amesema kuwa mara baada ya juhudi hizo kukamilika wataalamu tajwa watafahamishwa rasmi na hivyo kuwaomba wataalamu hawa na wadau wengine kuwa na subira.
“Tunapenda kuwafahamisha wahitimu ambao walikuwa hawajapangiwa vituo vya kufanyia mafunzo kwa vitendo, kuwa utaratibu unafanywa kuhakikisha kwamba wanapangiwa vituo hivi karibuni ambapo mtandao utafunguliwa na wahusika watapewa taarifa”. Amesema Prof. Muhammad Bakari
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)