Mataifa yenye wanafunzi werevu zaidi duniani



 Wanafunzi wa chuo kikuu cha Sydney, Australia

Katika kutathmini viwango vya elimu duniani, wengi wamekuwa wakiangazia sana ubora wa vyuo. Lakini kwa jumla, ni mataifa gani yenye wanafunzi walio bora zaidi?

Jambo la kushangaza ni kwamba orodha hii inaonyesha taswira tofauti sana na ile inayotolewa na utathmini wa vyuo vikuu.

Shirika la Kimataifa la Uchumi na Maendeleo (OECD) limefanya wazi matokeo ya mtihani wa kupima uwezo wa wanafunzi wanaohitimu kutoka nchi mbalimbali.
Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani?
Wanafunzi kuingia na bunduki darasani Texas, Marekani

Orodha ya ubora wa vyuo vikuu hutawaliwa na vyuo vikuu kutoka Marekani na Uingereza kama vile Harvard, MIT, Stanford, Oxford, Cambridge na UCL.

Lakini baada ya OECD kuchunguza uwezo wa kusoma na kuandika miongoni mwa wahitimu kutoka vyuo vikuu, wanafunzi walio bora zaidi ilibainika wanatoka Japan na Finland na wala si Marekani na Uingereza..

Nchi zenye wanafunzi bora zaidi wanaohitimu kwa mujibu wa OECD
Japan
Finland
Uholanzi
Australia
Norway
Ubelgiji
New Zealand
England
Marekani
Jamhuri ya Czech

Nchi hizi zote huwa mara nyingi hazina chuo haka kimoja kinachokuwa kwenye orodha ya vyuo vikuu 10 bora duniani.

Badala ya vyuo vikuu vya Marekani kufana, yamkini vyuo vikuu vya Norway na Australia vina wanafunzi bora wanaohitimu.

Kwa mujibu wa orodha ya ubora wa vyuo ya QS World University Rankings, kulikuwa na vyuo 32 vya Marekani katika 100 bora, na chuo kikuu kimoja pekee kutoka New Zealand.

Lakini ripoti ya OECD inaonesha wanafunzi wa New Zealand wanafanya vyema kushinda wenzao Marekani. Image
Oxford University
Oxford kilirodheshwa kuwa chuo kikuu bora duniani kwenye orodha ya gazeti la Times
Tokyo
 Wanafunzi waliohitimu kutoka Japan walifanya vyema zaidi tathmini ya OECD

Orodha ya ubora wa vyuo vikuu ya QS 2016-17
Massachusetts Institute of Technology (MIT)
Stanford University
Harvard University
University of Cambridge
California Institute of Technology (Caltech)
University of Oxford
University College London
ETH Zurich
Imperial College London
University of Chicago
 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top