KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm atoa msimamo juu ya soka la timu yake


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans-van-der-Pluijm
 
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema timu yake haijashuka kiwango kama ambavyo baadhi ya wadau wa soka wanavyodai na kuongeza kuwa muda si mrefu watarudi katika ubora
wao.

Baadhi ya wadau na wachambuzi wa soka kwa siku za karibuni wamekuwa wakitoa maoni yao kuwa Yanga imekwisha na wengine wakidai imechoka kutokana na wachezaji wengi kutopata muda wa kupumzika baada ya kutoka kwenye mashindano ya kimataifa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema muda sio mrefu watarudi tena na itadhihirika kama kweli wamechoka ama la.

“Sio kweli kama tumekwisha, tuko vizuri na muda sio mrefu mtaona mambo mazuri, tunaendelea kujipanga na kurekebisha mapungufu yetu kuhakikisha tunafanya vizuri,”alisema.

Yanga imetoka kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matokeo hayo yameishusha kutoka nafasi ya tatu hadi ya tano ikiwa na pointi 11 sawa na Azam FC ambao wanashika nafasi ya sita, lakini Yanga ikiwa nyuma mchezo mmoja.

Timu zinazoongoza nne bora ni Simba yenye pointi 17, Stand United 15, Mtibwa Sugar 13 na Kagera Sugar yenye pointi 12.

Kikosi hicho kilianza mazoezi juzi jioni kwenye uwanja wa Polisi Kurasini kujiwinda katika mchezo ujao dhidi ya Ruvu Shooting.

Bado timu hiyo na Simba zimekuwa zikihangaika kutafuta viwanja vyao vya nyumbani, baada ya ule wa taifa kuzuiwa kuutumia kufuatia vurugu zilizojitokeza katika mchezo wao uliopita.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top