Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi.




JESHI la Polisi nchini linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kuacha mara moja, kwani takwimu za makosa ya kujichukulia sheria mkononi yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi katika kipindi cha Januari hadi Agosti 2016 ni matukio 705.


Katika matukio hayo yaliyoripotiwa, Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 393.


Hayo yametolewa katika taarifa kwa waandishi wa habari na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi, ACP Advera Bulimba jijini Dar es Salaam leo.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa ni kosa kuzipuuza sheria za nchi zilizopo na wakati mwingine kuzikiuka kwa makusudi na mbaya zaidi baadhi yao kufikia hatua ya kuwaua watu wasio na hatia kwa hisia.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mwananchi yeyote anapaswa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mhalifu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka katika maeneo yao.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini, litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa kufuatilia na kuwakamata watu wote wanaojihusisha na tabia za kujichukulia sheria mkononi.


Jeshi la Polisi linatoa wito kwa watu wote wakiwemo wenye ushawishi mkubwa katika jamii kuendelea kukemea na kutoa elimu juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top