AUDIO: Mbao ilininyima usingizi – Pluijm





Kocha wa Yanga Hans van Pluijm amekiri timu ya Mbao FC ilikuwa ikimnyima usingizi kutokana na ubora wa timu hiyo amabayo imepanda kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu huu ikiwa ni msimu wake
wa kwanza.

Hans amesema Mbao ni miongoni mwa timu bora kwenye ligi msimu huu kwani licha ya kupoteza mechi bado walicheza kiufundi.

“Nilikuwa silali vizuri kwasababu nilikuwa najua ubora wa wapinzani wetu, wanaukuta mgumu na ilionekana namna walivyoanza kipindi cha kwanza. Walizuia vizuri, hakukuwa na nafasi ya kupitisha mipira.”

“Nimpongeze kocha wa timu pinzani licha ya kupoteza mchezo wamecheza vizuri kiufundi, walitaka kutumia mashambulizi ya kushtukiza, niliangalia mechi zao kadhaa zilizopita.”

“Kipindi cha kwanza kunawakati tulicheza kwenye nusu yao lakini pasi za mwisho hazikwenda vizuri, lakini kipindi cha pili tulishambulia sana goli lao. Tulipata goli kwa kosa la golikipa lakini ndivyo mchezo wa soka ulivyo ni mchezo wa makosa.” “Katika mchezo wa leo najivunia vijana wangu walipambana na walistahili ushindi dhidi ya miongoni mwa timu bora kwenye ligi.”






 




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top