Shiza Ramadhani Kichuya azungumzia goli lake lililoizamisha Azam








MSHAMBULIAJI wa Simba, Shiza Kichuya aliyepeleka furaha Msimbazi baada ya kufunga bao ambalo liliifanya Simba kuondoka na pointi tatu wakati ikipambana dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru.
Kichuya alipachika bao dakika ya 70 na kufanya awe na mabao mawili kwenye ligi msimu huu huku la kwanza akiwa alilifunga kwenye mchezo wa ufunguzi wa dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa.
Akizungumza baada ya mechi kumalizika alisema
“Kocha anatufundisha tukipata nafasi nje ya 18 tupige kwahiyo mimi nilipata nafasi nikaona ile ndiyo nafasi pekee nikapiga bahati nzuri nikafunga goli”,

“Najisikia faraja sana kwasababu kila siku napambana ili niwe nafunga magoli, nafurahi kufunga kwenye mchezo dhidi ya Azam na ntazidi kupambana ili niweze kufunga kwenye mechi zijazo.”

“Ushindi dhidi ya Azam umetufanya tuongoze ligi kwa kufikisha pointi 13, nafasi ya ubingwa ipo kila kitu kinawezekana na sisi tumekuja kupambana kuipatia mafanikio timu yetu.”

Winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amekuwa na mchango mkubwa tangu aliposajiliwa Simba akiwa ameshacheza kwenye kikosi cha kwanza mechi zote tano ambazo klabu yake imecheza msimu huu.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top