NDEGE mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada
ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 NextGen imetua saa 6:15 leo mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute). Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
PICHA 12 NDANI NA NJE ZA NDEGE MPYA BOFYA HAPA
Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais Dk John Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
PICHA 12 NDANI NA NJE ZA NDEGE MPYA BOFYA HAPA
Nafasi za kazi bofya hapa
Habari zilizopo katika magazeti ya leo Jumatano september 21, 2016 bofya hapa
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo jumatano september 21, 2016 bofya hapa
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)