Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Kilimanjaro, imemtia hatiani Diwani wa kata ya Pasua mjini Moshi kwa tiketi ya Chadema, Charles Mkalakala (47) kwa makosa mawili likiwamo la kumshambulia Polisi
.
.
Mbali na kumtia hatiani kwa kosa hilo, lakini mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi, Idan Mwilapo pia ilimtia hatiani diwani huyo na washirika wake wengine watatu kwa kosa lingine la kumzuia polisi huyo kufanya kazi yake.
Hukumu hiyo imetolewa leo ambapo kwa kosa la kumshambulia Polisi huyo, Diwani huyo alihukumiwa kulipa faini ya Sh 500,00 na kumlipa polisi huyo fidia ya Sh 400,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Katika kosa la pili lililomhusisha Diwani huyo na washitakiwa, Hussein Mkalakala (21), Fikra Said (23) na Raymond Andrea(34), Mahakama iliwahukumu kulipa faini ya Sh400,000 kila mmoja.
Video Mpya : Brown Mauzo Ft. Alikiba - 'Nitulize'bofya hapa
Video : Tox Star Ft. Barnaba - 'Chillax' bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Video : Tox Star Ft. Barnaba - 'Chillax' bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)