Burundi yamwaga msaada waathirika wa tetemeko la ardhi


 Serikali ya Burundi imetoa msaada wa vyakula kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera na kuvikabidhi kwa viongozi wa mkoa huo wakiongozwa na Naibu Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Suzan Kolimba aliyeiwakilisha Tanzania


Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana akikabidhi msaada huo leo wilayani Ngara amesema msaada ulitolewa na nchi hiyo ni mchele tani 100, mahindi tani 50, sukari tani 30 na majani ya chai tani tatu.


Nzeyimana amesema wakazi wa Kagera waliokumbwa na tetemeko hilo ni ndugu wa wananchi waliko nchini Burundi hivyo nchi imeguswa na na athari hiyo na kwamba msaada huo ni kidogo lakini upokelewe kwa lengo la kukuza mahusiano na ujirani mwema.
Nafasi za kazi bofya hapa




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top