Vyuo vikuu vilivyopokea fedha ambazo wanafunzi hawapo vyuoni vyapewa siku saba kurejesha fedha hizo



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo vikuu kurejesha fedha zilizopokea ambazo ni za wanafunzi ambao hawapo
chuoni.


Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi la uhakiki wa wanafunzi wanufaika wa mikopo vyuo vya Elimu juu.


Prof. Ndalichako amesema kuwa uhakiki wa wanafunzi hao umefanyika katika vyuo 31 kati ya vyuo 81 vilivyopo nchini.

Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.


“Mikopo ya Wanafunzi hao imesitishwa na kwa wale ambao ni wanafunzi halali lakini walishindwa kujihakiki itabidi waombe tena mkopo,” alifafanua Mhe. Ndalichako.


Ameendelea kwa kusema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/16 wanafunzi hao hewa wameigharimu Serikali kiasi cha shilingi 3,857,754,460.

Kutokana na mambo yaliyobainika Serikali imechukua hatua zifuatazo

Vyuo vikuu ambavyo vimepokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku saba kuanzia August 17 2016
Vyuo vya elimu ya juu vinaagizwa kuweka mfumo mzuri wa uhifadhi wa kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambapo fedha za mikopo hilipwa.
Vyuo vikuu vinaagizwa kuwasilisha bodi ya mikopo, kwa wakati taarifa zote za kitaaluma na za kibenki za wanafunzi ili kuiwezesha kufanya marekebisho stahiki katika kumbukumbu zao na kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za wanafunzi kama zilivyopelekwa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za waafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
Vyuo viweke utaratibu mzuri wa kudhibiti malipo kwa wanufaika wa mikopo ili kuepuka kufanya malipo kwa wanafunzi hewa.
Wakuu wa vyuo ‘VCs’ na Principals’ waweke mfumo wa kuhakiki usahihi wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa bodi ya mikopo na watawajibika kwa usahihi wa taarifa zinazowasilishwa kwani zoezi la uhakiki limebaini kuwepo kwa usdadanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi; wapo ambao hawakufanya mtihani au waliofeli lakini wameandikiwa PASS ili waendelee kupata mikopo.
Uchunguzi zaidi utafanyika kwa miaka iliyopita ili kubaini fedha za mikopo ambzo zimelipwa kwa watu wasiostahili. Hatua hii inatokana na matokeo ya uchunguzi ambao umebaini kuwa wapo baadhi ya wanafunzi waliohitimu tangu mwaka 2013 lakini wameendelea kupokea fedha na wengine waliofukuzwa kwa kushindwa masomo tangu mwaka 2013/14 lakini bado wamelipwa hadi mwaka 2015/16. 
 Azam Mabingwa Ngao ya Jamii bofya hapa


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top