Simbachawene awatumbua wawili Songwe na Mbeya


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene. 

 Maofisa elimu wawili katika mikoa ya Songwe na Mbeya wamesimamishwa kazi baada ya wanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Ileje kukutwa wamelala chini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene ndiye amewasimamisha vigogo hao.


Waliotumbuliwa ni Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Mwalimu Charles Mwakalila na Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ileje, James Milanzi, ambao wanatuhumiwa kutoisimamia vizuri shule hiyo.


Waziri Simbachawene amesema jana kuwa ameamuru Mwalimu Mwakalila asimamishwe kwa sababu ndiye alikuwa anasimamia shule zote za mikoa ya Mbeya na Songwe wakati wanafunzi hao wanapokewa kabla ya utawala wa mikoa hiyo haujagawanywa.



Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top