Sababu kwanini Paul Pogba amefungiwa kucheza vs Bournemouth


​Kiungo mpya wa Manchester United Paul Pogba amesimamishwa kuitumikia timu yake kwa mchezo wa kwanza wa Premier League, chama cha soka cha England kimethibitisha
Pogba, 23, alirejea Old Trafford kutoka Juventus kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya £89.3 million, miaka 4 baada ya kuhamia klabu ya Turin kwa ada ya £800,000 kufuatia kukosa muda wa kucheza na mgogoro wa mkataba mpya. 

Hata hivyo Pogba itambidi asubiri mpaka wiki ijayo kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu yake mpya kwa sababu amefungiwa kucheza mchezo wa Jumapili dhidi ya Bournemouth.


Kiungo huyo wa Ufaransa amesimamishwa kwa kosa la kupata kadi mbili za njano katika msimu uliopita wa mashindano ya Coppa Italia, na adhabu yake imehamia katika michezo inayosimamiwa na Chama cha soka cha England.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top