Ratiba ya nusu fainali ya Michuano klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho imetoka

Ratiba ya nusu fainali ya Michuano klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho imetoka, ambapo kwa upande wa Kombe la Shirikisho, TP Mazembe itamenyana na Etoile du Sahel ya Tunisia, huku MO Bejaia ya Algeria wataumana uso kwa uso na waarabu wenzao wa FUS Rabat ya Morocco.

Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa, ambapo bingwa wa michunao hiyo anatarajiwa kujizolea kitita cha dola za Kimarekani Milioni 1.5 pamoja na kupata tiketi ya kucheza Klabu Bingwa ya Dunia, Mabingwa wa zamani Zamalek ya Misri ambao wamechukua kombe hilo mara tano watamenyana na vigogo wa Morocco, Wydad Casablanca kuwania kutinga fainali.

Ikumbukwe kuwa Zamalek watakuwa na ari kubwa kutokana na kuikosa hatua hii kwa takriban miaka 10, baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 2005.

Zesco United ya Zambia, ambao walimaliza kwenye nafasi ya pili kwenye kundi A nyuma ya Wydad Casablanca, watapambana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Zesco ambao wanacheza hatua hii kwa mara ya pili kwenye historia ya klabu yao, watakuwa na shughuli pevu mbele ya Wazulu hao wa Mamelodi ambao kwa hakika kwenye michunao ya mwaka huu wamekuwa kwenye kiwango bora sana
.
Klabu Bingwa

Sept 16-18, 2016
Zamalek (Misri) Vs Wydad Athletic Club (Morocco)
Zesco (Zambia) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

Kombe la Shirikisho

Sept 23-25, 2016
TP Mazembe (DRC) Vs Etoile du Sahel (Tunisia)
MO Bejaia (Algeria) Vs FUS Rabat (Morocco) 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top