Pogba ana kiporo alichobakiza Old Trafford – na hivi ndio Man Utd ilivyoshinda Barca na Madrid


​ Paul Pogba bado hajasaini mkataba wa kujiunga na Manchester United, lakini anataka kujiunga na klabu aliyowahi kuichezea na klabu hiyo pia inamhitaji
Sio kwa mara ya kwanza, uhamisho mkubwa unachukua muda mrefu kukamilika, United wametulia na wanajiamini. Wangekuwa na wasiwasi kama muda wa usajili ungekuwa unakaribia kumalizika, lakini muda unaruhusu, kuna taratibu nyingi zinatakiwa kukamilika kabla ya makubaliano hayajafikiwa rasmi. Siku hizi, uhamisho mkubwa kama huu hahusishi kusaini mkataba tu, kuna mambo mengi ya kuweka sawa, ikiwemo masuala ya masoko na haki za taswira.

United wamekuwa karibu na kutangaza usajili wa Pogba kwa mara kadhaa wiki iliyopita, lakini bado uhamisho haujawa rasmi, na mashabiki wamekuwa wakishangaa nini tatizo, wakati baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakihisi labda kuna story nyingine inayosababisha hajasaini.





Kwa mashabiki wa United, uhamisho wa Pogba umetawala sana dirisha hili la usajili, kama ilivyokuwa wakati wakihusishwa na usajili wa Alan Shearer mwaka 1996 na Wesley Sneijder mwaka 2011. Wote hawa waliishia kwenye vilabu vingine badala ya Old Trafford; Shearer alichagua klabu ya nyumbani kwao Newcastle, ambao walilipa rekodi ya dunia wakati ya kiasi cha £15 million, wakati masuala ya kifedha yalikwamisha uhamisho wa Sneijder.

United hawakuwa na uhakika wa kuwasaini Shearer wala Sneijder, lakini kwa Pogba tofauti, hata kama imekuwa jambo linalochukua muda mrefu, limekuwa jambo kubwa kutokana na ukweli kwamba Pogba ni mchezaji ambaye amekuwa akihusishwa na vilabu vikubwa na tajiri tangu alipoanza kung’aa na Juventus.





Mwanzoni mwa mwaka huu, uhamisho wa kuondoka nchini Italy ulianza kuwa na mashiko, hata kama baadhi ga wachezaji wenzie wa Juve waliamini Pogba anataka kubaki Turin na kuwa sehemu ya kikosi cha kushindania ubingwa.


Vilabu vya England na Spain na Ufaransa vilitajwa sana, Real Madrid, Barcelona, PSG na vilabu vya mji wa Manchester vyote vilihusishwa.

Kuelekea kujenga upya kwa dimba la Camp Nou, Barca walikuwa wamepoteza uwezo wa kiuchumi wa kumsaini Pogba. MADRID walikuwa wakipewa nafasi kubwa zaidi, walikuwa wametoka kubeba ubingwa wa ulayana kocha wao Zinedine Zidane, mfaransa mwenzie na mmoja wa mashujaa wa utotoni wa Pogba. Zidane alikuwa anamhitaji Pogba ahamie Madrid kutokea Juve kwa ada ya uhamisho wa dunia, kama ilivyokuwa yeye mnamo mwaka 2001 kwa ada ya €75m.





United executive vice-chairman Ed Woodward alisema miaka 3 iliyopita kwamba klabu yake haitoshindwa vita vya bei za kuzasajili vipaji vikubwa. Woodward amekuwa ndio mtu anayelipigania dili la Pogba, alisafiri kutoka Manchester mpaka Florida kukutana na mchezaji na wakala wake mwezi uliopita.



Wakati fedha haiwezi kuwa kikwazo, kuna mawazo ya kwamba kuna sehemu nzuri za kuishi kuliko Manchester, au kunaweza kuwa mazingira mazuri ya kodi katika nchi nyingine. Au kuna timu nzuri zaidi ya United, ambao walimaliza msimu uliopita katika nafasi ya 5. Kurudi katika klabu yake ya zamani halikuwa chaguo la kwanza la Pogba mpaka kufikia miezi kadhaa iliyopita.





Klabu iliamua kuwekeza ushawishi wake katika mambo chanya zaidi katika mazungumzo, walisisitiza katika size ya ukubwa klabu na namna itakavyoweza kumkuza mchezaji huyo na taswira yake. Pia walitumia kigezo cha ukweli kwamba Pogba angekuwa mchezaji 3 kwa ukubwa katika klabu ya Madrid – Cristiano Ronaldo wa kwanza kisha Bale, then angekuja yeye.

Hivyo kwa upande wa United, ikiwa Pogba angejiunga nao, wangemfanya yeye namba 1.Timu itaundwa kumzunguka na jina lake litakuzwa mno kibiashara. Hili liliwafurahisha Adidas, ambao alisaini nao mkataba wa thamani ya €40m mnamo March akikataa mkataba wa Nike. United pia wana biashara na Adidas.


Watengenezaji wa vifaa vya michezo wa kijerumani wamekuwa wapesi kutoa ishara za usajili ili kuwavutia mamilioni yawatu wanaowafuatilia taarifa za usajili. Viashiria vingi vimekuwa vikichukua nafasi katika mitandao ya kijamii na idadi ya followers ya Pogba imekuwa kwa asilimia 25 tangu alipoanza kuhusishwa na United.

United wamekuwa ni moja ya vilabu vya mwisho kukumbatia ulimwengu wa mitandao ya kijamii – lakini katika miaka ya hivi karibuni wameanza kujiingiza kwenye mitandao hii.

Uwepo wa klabu mitandaoni ni sehemu muhimu wakati klabu inapokuwa ikijadiliana na washirika wa kibiashara kama Richard Arnold, ambaye ni mtu wa pili kimamlaka baada ya Woodward, anavyoelezea wanavyoweza kuwasiliana kila siku.

Wachezani wamekuwa wakitumia kurasa zao kupost matangazo ya kibiashara ya wadhamini wa klabu, na hili limesaidia kukua kwa idadi ya wadhamini wa klabu.

Uhamisho wa wachezaji pia imekuwa kama sehemu ya kujionyesha mbele ya hadhira. . Mnamo January 2014, Juan Mata aliwasili Carrington na helicopter kwenda kusaini mkataba wa kujiunga na United kwa ada iliyovunja rekodi kipindi hicho ya £37.1m. Sasa, kwa mara nyingine tena United wanataka kuvunja rekodi ya dunia.

Wakati itakapotangazwa, tegemea habari kubwa zaidi za kutengeneza attention na vichwa vya habari vikubwa. Mashabiki wanapenda, hasa vijana, wakati wadhamini wanapoona logo zao zikionekana kwa ukubwa huo wanafurahia, hasa ukizingatia mvuto wa ligi ya England, habari zake zinakuwa kubwa na kusafiri mbali zaidi katika maeneo tofauti duniani. United sio tena ni ya jiji la Manchester tu, ni jambo/kitu cha kidunia, wakiwa na ofisi kubwa sana London na Unuted United States pamoja na Hong Kong.

Mara tu itakapokuwa rasmi kuhusu Pogba, tegemea promotions na matamko makubwa na kuja kwake kutatengenezwa kibiashara.




Yote kwa yote, Pogba ana biashara ambayo haikumaliza ndani ya Manchester. Muda huu ndio huu wa kuiteka dunia ukizingatia utawala wa CR7 na Messi huenda ukawa unaelekea mwishoni. Dunia itahitaji mashujaa wapya. Pogba ni mmojawapo. 
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top