MAJIBU YA MOURINHO KWA KLOPP, WENGER, JUU YA PAUNDI MIL 100 ZA USAJILI WA POGBA


Jose Mourinho amewatuhumu mahasimu wake kwenye soka Arsene Wenger na Jurgen Klopp kwamba hawana maadili baada ya kukosoa uamuzi wa United kuhusishwa na ununuzi wa Paul Pogba kwa ada ya paundi mil 100.

Mourinho amejibu mapigo baada ya Wenger kusema kwamba ni ‘upuuzi wa hali ya juu’ kutumia pesa nyingi kiasi hicho kununua mchezaji.

Mourinho ana matarajio makubwa ya uhamisho wa Pogba kukamilika wiki ijayo na Mreno huyo ambaye ataiongoza United kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City kesho, ameghadhabishwa na kitendo cha makocha hao kuingilia masuala yasiyowahusu.

Alisema: “Mimi naongea yanayohusu klabu yangu tu. Tayari nimewasikia wenzangu wawili kutoka klabu nyingine wakituongelea sisi. Mimi sipendi mambo hayo. Sio vizuri kimaadili.

“Kuna baadhi ya mambo ambayo nikifanya nitakuwa nimeenda kinyume cha misingi ya kazi yangu, lakini wengine wakifanya basi ni kawaida tu, hakuna anayezungumza chochote. Wanafanya lolote wawezalo. Biashara yetu ilikuwa ni nzuri.

“Tumefanya maamuzi, tumeamua kuleta wachezaji wanne na sio kumi, hiyo ndiyo level ya Manchester United. Kwahiyo nadhani tunaweza kuimarisha kikosi na hatutaongeza yeyote mwingine. Huu ndio utaratibu wetu.”

Alipoulizwa kama aliongea hivyo kumlenga Klopp, Mourinho alijibu: “Nisingeoenda kuzungumza chochote, uko sahihi, alikuwa ni mmoja wao lakini sitaki kuzungumza chochote. Ameongea yanayotuhusu lakini nisingependa kuongea kuhusu yeye au timu yake.

“Tumefanya maamuzi, tumeamua kuleta wachezaji wanne na sio kumi, hiyo ndiyo level ya Manchester United. Kwahiyo nadhani tunaweza kuimarisha kikosi na hatutaongeza yeyote mwingine. Huu ndio utaratibu wetu.”

“Beki kijana anahitaji kutengenezwa kuwa wa kiwango cha juu lakini licha ya kuwa na kiwango bora.

“Tuna mchezaji mbunifu ambaye tunaufahamu ubora wake, mshambulizi bora, na tunaeelekea kupata kiungo bora. Tunajaribu kubalansi timu. Nina furahha na kikosi changu, nafurahia juhudi zinazofanywa na klabu yangu. Wengine watajijua wenyewe na matatizo yao.”

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top