Mawaziri wa Machar wafutwa kazi Sudan Kusini

 Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametoa amri ya kufutwa kazi mawaziri wote wa aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Vikosi vinavyowatii viongozi hao wawili vilihusika katika mapigano mapya mnamo mwezi
Juni na kuwawacha mamia wakiwa wamefariki na maelfu bila makao.
Baada ya kukubaliana kuhusu kusitisha vita,bw Machar alienda mafichoni na mahala pake pakachukuliwa na Taban Deng ambaye alikuwa waziri wa madini,hatua ambayo Machar anasema ni kinyume cha sheria.
Mawaziri ambao wamefutwa kazi ni.
1. Alfred Ladu Gore, waziri wa maswala ya ndani
2. Duk Duop Bichok, Waziri wa mafuta
3. Dr Peter Adwok Nyaba, Waziri wa Elimu ya juu ,Sayansi na Teknolojia
4. Peter Marcello Nasir Jelenge, Waziri wa Leba,Huduma ya uma
5. Mary Alfonse Lodira, Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya mijini.
6. Mabior Garang de Mabior, Waziri wa Maji na kilimo cha Unyunyizaji.




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top