MANJI ATEUA KAMATI YA MASHINDANO


 

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ametangaza kamati mpya ya mashindano ambayo imeanza kazi yake mara moja.

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedith amethibitisha kuteuliwa kwa wajumbe
wa kamati hiyo.

“Mwenyekiti amevunja rasmi kamati ya mashindano iliyokuwa chini ya mjumbe wa kamati ya utendaji iliyopita Mhandisi Isack Chanji mara moja kuanzia leo, Mwenyekiti wa Yanga kwa mamlaka aliyonayo ya kuteua wajumbe watatu wa kamati ya utendaji amemteua Mhandisi Paul Malume kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji mpya na pia kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya mashindano mara moja kuanzia sasa” amethibitisha Deusdetith kaimu Katibu mkuu wa Yanga.

Kamati mpya ya mashindano ambayo Mwenyekiti wake ni Paul Malume inaundwa na wajumbe walioteuliwa ambao ni;
Mustafa Ulungo
Eng. Mahende Mugaya
Abdallah Bin Kleb
Jackson Maagi
Samwel Lukumay
Hussein Nyika
Athumani Kihamia (kutoka Arusha)
Felix Felician Minde (kutoka Mwanza)
Leonard Chinganga Bugomola (kutoka Geita)
Omary Chuma
Hussein Ndama
Hamad Ali Islam
Yusuphed Mhaden
Beda Tindwa
Moses Katabalo
Roger Lamlembe

Kwa maana hiyo, Mhandisi Isack Chanji atabaki kuwa mshauri kamati hiyo mpya ya mashindano.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top