MAAMUZI MAPYA KUHUSU KESSY KUITUMIKIA YANGA


Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji imelipitisha jina la mlinzi wa kulia wa Yanga Hassan Kessy Ramadhani kuitumikia klabu hiyo baada ya hapo awali kuwepo na mvutano mkubwa na klabu yake ya zamani Simba SC.

Simba ilikuwa ikimtuhumu Kessy kuvunja mkataba kwa kuanza kuvaa jezi, kufanya mazoezi, kusafiri na kushiriki shughuli mbalimbali za mabingwa hao wa VPL msimu uliopita wakati muda wa mkataba wake na Wekundu hao wa Msimbazi haujafika kikomo.

Kutokana mgogoro huo, klabu ya Simba haikutoa barua (release letter) kumruhusu Kessy kuitumikia Yanga ikidai kulipwa fidia na mchezaji huyo kwa kuvunja mkataba. Sakata hilo lilimfanya Kessy kushindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga katika michuano ya kimataifa licha ya kuendelea kufanya mazoezi na kikosi cha Hans van Pluijm.

Uamuzi huo unamfanya Van Pluijm kuwa huru kumtumia Kessy kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara kuanznia msimu mpya wa 2016/17 pamoja na ile michuano ya kimataifa ambayo Yanga wataiwakilisha Tanzania kwenye klabu bingwa Afrika.

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji awali ilikuwa ikutane Jumanne lakini ilishindikana na baadae zikatoka taarifa kwamba, wachezaji wote walioombewa leseni na vilabu vyao wataruhusiwa kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Jumatano kati ya Yanga na Azam huku Kessy aliitumikia Yanga.

Leo Ijumaa August 19 taarifa zimetoka kwamba Kessy yuko huru kuitumikia Yanga baada ya kamati hiyo kukaa na kupitia kesi zote za usajili ikiwemo ya Kessy.
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumamosiu August 20, 2016 bofya hapa










 Azam Mabingwa Ngao ya Jamii bofya hapa




MANJI AJIUZULU YANGA bofya hapa





Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top